Bibi Peng Liyuan ahutubia ufunguzi wa mkutano wa WHO kuhusu kutokomeza vifo vya wagonjwa wa UKIMWI kutokana na kifua kikuu
2021-06-08 08:47:59| CRI

Mke wa rais wa China Bibi Peng Liyuan jana Jumatatu alitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa Shirika la Afya Duniani WHO kuhusu kutokomeza vifo vya wagonjwa wa UKIMWI kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu (TB).

Bi. Peng Liyuan amesema China imejenga utaratibu wa ushirikiano kati ya taasisi za kinga na tiba ya UKIMWI na Kifua Kikuu, hali ya maambukizi ya UKIMWI imedhibitiwa katika kiwango cha chini, na katika miaka 20 iliyopita kiwango cha maambukizi na vifo kutokana na Kifua Kikuu kimepungua kwa asilimia 40 na asilimia 70 mtawalia. Amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na juhudi za pamoja za serikali, wahudumu wa afya na watu wanaojitolea.

Bibi Peng ametoa wito kwa nchi mbalimbali na watu wa sekta mbalimbali kuungana mkono na kuchukua hatua kuimarisha kazi ya kukinga na kutibu UKIMWI na Kifua Kikuu, na kufanya juhudi kwa ajili ya kujenga jumuiya ya binadamu kwenye sekta ya afya.