Biden abatilisha amri za Trump dhidi ya TikTok na Wechat
2021-06-10 08:51:32| CRI

Rais Joe Biden wa Marekani jana Jumatano alibatilisha na kubadilisha amri za utendaji alizosaini rais wa zamani Donald Trump dhidi ya TikTok, WeChat na App nyingine nane.

Amri mpya iliyosainiwa na Rais Biden jana inaiagiza Wizara ya Biashara ya Marekani kutathmini App zinazohusiana na “wapinzani wa kigeni” chini ya kanuni za usalama wa mnyororo wa ugavi wa Marekani, na kuchukua hatua ipasavyo.

Amri hiyo pia inaitaka Wizara ya Biashara ya Marekani kuweka machaguo ya kulinda data nyeti binafsi na kutatua “tishio linalowezekana” kutoka kwa App husika.