Uingereza na Marekani zakubaliana kufungua usafiri kati yao baada ya Johnson na Biden kukutana
2021-06-11 09:03:50| CRI

Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson na Rais Joe Boden wa Marekani wamekubaliana kurudisha usafiri kati ya nchi hizo mbili na kusaini makubaliano ya Atlantiki, muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa kundi la G7.

Msemaji wa Ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza amesema kwenye taarifa kuwa viongozi hao wamekubaliana kurudisha usafiri kati ya nchi zao na kubadilishana taarifa zitakazosaidia kupambana na virusi vya Corona kwenye nchi zao na kimataifa.

Kupitia makubaliano hayo ya Atlantiki ambayo msingi wake ni yale yaliyosainiwa mwaka 1941 na viongozi wa nchi hizo, yanalenga ushirikiano kwenye nyanja mpya ikiwa ni pamoja na fedha haramu, migogoro na msimamo mkali, mabadiliko ya tabia nchi, na misukosuko ya afya ya umma duniani kama janga la COVID-19.

Rais Joe Biden yuko nchini Uingereza kwa ajili ya mkutano wa kundi la G7 unaoanza leo.