Manowari mbili za Iran zimeingia kwenye bahari ya Atlantiki kwa mara ya kwanza
2021-06-11 09:04:22| CRI

Kamanda mwandamizi wa jeshi la Iran Habibollah Sayyari, amesema manowari mbili za Iran zimeingia kwenye bahari ya Atlantiki kwa mara ya kwanza.

Manowari hizo mbili, moja ikiwa imetengenezwa na Iran yenyewe ziling’oa nanga kutoka Bandari ya Abbas Iran na kuingia kwenye bahari ya Atlantiki bila kupita kwenye bandari ya nchi nyingine. Kamanda huyo amesema jeshi la Iran linachukulia uwepo wake kwenye bahari ya kimataifa kuwa ni haki yake, na litaendelea kufanya hivyo kwa nguvu.

Vyombo vya habari vya nchi za magharibi vimesema manowari hizo za Iran zinaelekea Venezuela, na gazeti la Politico la Marekani limesema serikali ya Rais Biden imezitaka Venezuela na Cuba kuzitaka manowari hizo zirudi, ikiamini kuwa zimebeba silaha zinazopelekwa nchini Venezuela.