Idadi ya watu wa Xinjiang yaongezeka kwa asilimia 18.5 katika muongo uliopita
2021-06-14 15:20:28| Cri

Idadi ya watu katika mkoa unaojiendesha wa kabila linalojiendesha wa Uyghur wa Xinjiang imeongezeka kwa asilimia 18.5 toka mwaka 2010 hadi mwaka 2020, hii ni kwa mujibu wa sensa ya saba ya taifa.

Hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka jana, idadi ya wakazi wa kudumu wa Xinjiang imefika milioni 25.85, likiwa ni ongezeko la watu milioni 4.04 tangu ilipofanyika sensa ya sita mwaka 2010. Ongezeko la idadi ya watu mkoani humo katika muongo mmoja uliopita lilikuwa asilimia 13.14 ambalo ni kubwa kuliko wastani wa taifa. Idadi ya watu wa kabila la Uyghur imeonegezeka kwa watu milioni 1.62 likiwa ni ongezeko la asilimia 16.2 zaidi kuliko muongo mmoja uliopita.

Takwimu pia zinaonesha kuwa ongezeko lililotulia la idadi watu limechangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya mkoa huo, na katika miaka ya hivi karibuni mkoa wa Xinjiang umevutia wawekezaji kufanya biashara mkoani humo, kutokana na mazingira yenye utulivu na masikilizano.