China kusaidia nchi za Kiisalamu barani Afrika kukabiliana na COVID-19
2021-06-17 09:34:25| CRI

 

 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema China imesaini makubaliano na Benki ya Maendeleo ya Kiislamu iliyo chini ya Shirika la Ushirikiano la Kiislamu, ili kuongeza ushirikiano katika kukabiliana na janga la COVID-19.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, China itaunga mkono nchi 11 za Kiislamu barani Afrika kununua vifaa vya maabara, na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi, ili kuongeza uwezo wa kupambana na janga hilo.

Zhao amesema, tangu kutokea kwa janga la COVID-19, China na nchi za Kiislamu zimesaidiana na kushirikiana vizuri, na kuwa mfano mzuri wa kukabiliana na janga hilo kwa pamoja. Amesisitiza kuwa China inatilia maanani sana uhusiano wake na Shirika la Ushirikiano la Kiislamu, na inapenda kuhimiza uhusiano huo kuwa na kiwango cha juu zaidi.