Mazungumzo ya kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran yapata maendeleo
2021-06-21 08:18:22| Cri

Mazungumzo ya kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 (JCPOA) yamepata maendeleo na kukaribia kufikia makubaliano.

Naibu katibu mkuu wa idara ya mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya siasa Enrique Mora amesema hayo baada ya mkutano wa Kamisheni ya Pamoja ya JCPOA uliohudhuriwa na wawakilishi kutoka China, Ufaransa, Ujerumani, Russia, Uingereza na Iran, na kuongeza kuwa, bado itachukua muda kufikiwa kwa makubaliano kamili.

Amesema maendeleo yamepatikana katika masuala mbalimbali ya kiufundi na wamefahamu kwa kina zaidi nyaraka za kiufundi ambazo zina utata, jambo ambalo pia linaruhusu kupatikana kwa mawazo sahihi juu ya masuala ya kisiasa yaliyopo.