Korea Kaskazini yasisitiza hakuna uwezekano wa kufanya mazungumzo yoyote na Marekani
2021-06-24 08:40:36| Cri

Korea Kaskazini imerejea tena msimamo wake kuwa, hakuna uwezekano wa kufanya mawasiliano na Marekani, kwani kufanya hivyo ni kupoteza muda.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini Ri Son Gwon ametoa taarifa akisema, wizara yake inapongeza taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na naibu mkurugenzi wa idara ya Kamati Kuu ya Chama cha Wafanyakazi nchini humo, Kim Yo Jung, ambayo imefuta matumaini na lawama za Marekani.

Katika taarifa yake, Kim Yo Jong alisema, ni makosa kwa Marekani kutarajia kurejesha mazungumzo na Korea Kusini.