Wataalamu wa anga za juu watembelea vyuo vikuu mkoani Hongkong na kuwataka wanafunzi wawe wazalando
2021-06-24 14:37:29| cri

Mwanachama wa Akademia ya Uhandisi ya China na msanifu mkuu wa vyombo vya anga za juu vya Shenzhou Qi Faren jana huko Hongkong amesema anatumai kuwa moyo wa safari za anga za juu utashawishi vijana wa Hongkong wawe wazalendo na kuchangia maendeleo ya nchi.

Kuanzia jana Jumatano, vikundi vya wataalamu wa anga za juu wa China watatembelea vyuo vikuu viwili na shule sita za sekondari mkoani  Hongkong kwa nyakati tofauti. Wakiwa katika shule na vyuo hivyo, wataalam hao watafanya semina, ili kuwashawishi wanafunzi vijana wawe na shauku ya kufanya      utafiti wa sayansi na kuwajengea kujiamini na uwezo wa teknolojia na sayansi wa China.

Wataalamu watakaoshiriki kwenye ziara hiyo ni pamoja na msanifu mkuu wa roketi za Long March Long Lehao, msanifu mkuu wa chombo cha kupeleleza sayari ya Mars Tianwen-1 Sun Zezhou, msanifu mkuu wa saitelaiti ya Beidou-3 Xie Jun na mkurugenzi mtendaji wa mradi wa chombo cha kutua Mwezini cha Chang’E-4 Zhang He.