China yaitaka Israeli kusimamisha ujenzi wa makazi katika eneo linalokaliwa na Wapalestina
2021-06-25 08:16:42| Cri

Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ametaka pande zinazohusika kujizuia katika kanda ya Gaza na kutoa wito kwa Israeli kusimamisha ujenzi haramu wa makazi katika eneo linalokaliwa na wapalestina.

Balozi Zhang amesema, ndani ya mwezi mmoja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupongeza kusimamisha mapambano kati ya Israeli na Palestina, serikali ya Israeli imeidhinisha maandamano ya bendera katika Mji wa Kale wa Jerusalem, hatua iliyoongeza mvutano, na Israeli kwa mara nyingine ilifanya mashambulizi ya anga huko Gaza, vitendo vinayoathiri usimamishaji wa vita ambao umekuwa dhaifu.

Pia amesisitiza kuwa, China inaihimiza Israeli kuzingatia Azimio No.2334 la Umoja wa Mataifa, kusimamisha kubomoa nyumba za Wapalestina, na kudhibiti kuongezeka kwa vurugu za wakazi wa huko.