Nchi zinazoendelea zaiunga mkono China katika kikao cha Baraza la haki za binadamu la UM
2021-06-28 10:08:26| CRI

Kikao cha 47 cha Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kinaendelea, na hivi karibuni nchi nyingi zimeeleza uungaji mkono kwa China katika masuala yanayohusu Xinjiang, Hong Kong na Tibet, huku zikipinga uingiliaji wa nje katika mambo ya ndani ya China.

Grenada imesaini hotuba ya pamoja ya kuunga mkono China iliyotolewa na Belarus kwenye kikao hicho, huku idadi ya nchi zilizosaini hotuba hiyo ikifikia 66.

Madagascar imetoa hotuba kwenye kikao hicho ikipongeza juhudi za serikali ya China katika kuhakikisha haki za uchumi, jamii na utamaduni za watu wake, na kusisitiza kuwa kushughulikia suala la haki za binadamu kunatakiwa kuhakikisha kunafuata ukweli bila upendeleo, kuacha kutumia vigezo viwili na wala kutolifanya liwe la kisiasa.

Chad imesema inaiunga mkono China kutekeleza sera ya “Nchi Moja, Mifumo Miwili” huko Hong Kong, huku ikisisitiza kuwa suala la haki za binadamu linapaswa kushughulikiwa kwa usawa na bila upendeleo, kwa kuheshimu mamlaka ya nchi na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.