Rais wa China awataka wanachama wa CPC watoe kipaumbele kwa maslahi ya umma
2021-06-29 11:11:41| CRI

Rais Xi Jinping wa China amewataka wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC kutoa kipaumbele kwa maslahi ya umma, kuendelea kuzingatia na kushughulikia kwa makini mahitaji ya umma, na kuwa pamoja na umma kama ndugu.

Rais Xi amesema hayo leo hapa Beijing kwenye hafla ya kutoa “nishani ya Julai mosi”, ikiwa ni heshima ya juu kabisa ya CPC. Amesisitiza kuwa wanachama wote wanatakiwa kujizatiti kikamilifu, kujitolea kwa nguvu zote na kuleta mafanikio bila kukidhalilisha Chama na umma na karne hii.