Sura ya Chama – Mwalimu Zhang Guimei
2021-06-29 14:47:38| cri

 

 

Zhang Guimei, ambaye ametumia miaka yake yote ya kazi kuwafundisha wasichana walio katika maeneo ya vijijini mkoani Yunnan, ameonesha jinsi roho ya kuwa mwanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China inarithishwa kizai baada ya kizazi.

“Mimi ni Zhang Guimei. Ni katibu wa tawi la Chama na mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Huaping iliyoko Lijiang. Shule yetu inatoa elimu ya bure kwa watoto wa kike wanaoishi milimani.”

Zhang Guimei ni mmoja wa timu ya wasichana walio maeneo ya milimani katika Kaunti ya Huaping, moja ya kaunti masikini zaidi nchini China.

Mwaka 1974, Zhang, akiwa na miaka 17, alikwenda Yunnan kujibu wito wa taifa wa kusaidia wakati katika maeneo yaliyo ndani zaidi. Alikwenda chuo na baadaye kufundisha akiwa na mumewe ambaye kwa bahati mbaya alifariki mwaka 1994 kutokana na maradhi ya saratani. Akiwa hana pesa wala mtoto, Zhang aliomba kuhamishiwa Huaping, ili kukwepa kumbukumbu zilizokuwa katika mji wa Dali. Miezi sita vaadaye aligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi, na wakazi wa huko walimchangia ili kuweza kulipia matibabu yake. Anasema upendo wa watu hao ulimpa ari ya kuishi.

Mwaka 2001, Zhang alipata wadhifa wa kuwa mkurugenzi wa kituo cha Yatima cha Huaping, ambapo idadi kubwa ya yatima walikuwa watoto wa kike. Anasema aligundua kuwa idadi ya watoto wa kike wanaoacha shule ilikuwa kubwa, na wakati mwingine, waliacha kwenda shule bila ya kutoa taarifa. Kutokana na hilo, aliamua kuondoa vizuizi vinavyowakabili watoto hao kadri anavyoweza, na mwaka 2008, alianzisha shule yake mwenyewe ya wasichana, ambapo wanasoma bure bila ya kulipa ada wala mahitaji ya kujiandikisha.

Waalimu wengi walidhani lengo la Zhang halitaweza kutimia, na miezi sita baadaye, nusu ya wafanyakazi katika shule hiyo waliacha kazi, lakini sita kati ya nane waliobaki, wote walikuwa wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China. walijipa moyo wakisema, “Hili ni jukumu na wajibu wa wanachama wa CPC. Sisi wanachama wa CPC ndio tunafanya kazi kwa ajili ya furaha ya watu kwa kufanya kazi ngumu zaidi? Hii ndio maana halisi ya kuwa mwanachama wa CPC”

Wafanyakazi hao waliobaki walijitahidi kadri wanavyoweza kutimiza malengo ya shule hiyo. Zhang mwenyewe alihamia shuleni hapo na kuishi pamoja na wanafunzi wake. Juhudi hizo zilizaa matunda, na katika miaka 13 iliyopita, shule hiyo imepeleka wasichana 1,800 katika vyuo vikuu.

Lakini miaka mingi ya kazi ngumu sasa inamzidi nguvu Zhang., ambaye sasa anategemea dawa na imani yake aliyoishikilia kwa muda mrefu kusonga mbele.

Zhang anasema, alipokuwa mtoto kaskazini magharibi mwa China, nyumba yao ilianguka baada ya theluji kuyeyuka wakati wa kipindi cha kutoka baridi kuelekea mchipuko, na mama yake alikuwa ndani. Watu wengi walikuwa nje wakifukua wakijaribu kuokoa watu, na alishindwa kupenya kwenye umati wa watu. Lakini watu wote waliokolewa. Anakumbuka msichana aliyekuwa na umri wa miaka 20 na zaidi kidogo, alimwambia baba yake atafute sehemu nyingine ya kujihifadhi kwa muda na arejee baada ya siku tatu, kwani katika kipindi hicho, nyumba yao itakuwa imeshajengwa upya. Na siku tatu baadaye, nyumba yao ilikuwa imekarabatiwa vizuri, baba yake alipotaka kumshukuru, msichana huyo alisema, “Huna haja ya kunishukuru, Ni wajibu wangu kwa kuwa mimi ni mwanachama wa CPC”. Zhang anasema alishangazwa sana, na hapo ndipo aliposhawishika zaidi na kupata nia thabiti, na anasisitiza kuirithisha kwa kizazi kingine, kwa wasichana anaowafundisha, na kwa wale ambao maisha yao yamebadilika daima.

Barua kutoka kwa wanafunzi wake inaonyesha kuwa amefanikiwa.

“Mpendwa Mwalimu Zhang, ninaondoka sasa. Nitarithisha wema niliopata kutoka hapa na kuupeleka sehemu za mbali. Nitatoa uzoefu wa kile kilichonigusa kwa wale nitakaokutana nao.”