Mkutano mkuu wa kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa CPC kufanyika hapa Beijing
2021-06-30 13:31:24| CRI

Mkutano mkuu wa kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) utafanyika kesho saa mbili asubuhi kwenye Uwanja wa Tian’anmen mjini Beijing, China.

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, Xi Jinping, ambaye pia ni rais wa China, na mwenyekiti wa Baraza la Kijeshi la Kamati Kuu ya CPC atahudhuria na kuhutubia mkutano huo.