Kamati Kuu ya Chama yawatunuku nishani wanachama waliotoa mchango mkubwa
2021-06-30 15:19:09| CRI

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China. Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China imewatunuku nishani wanachama wa Chama hicho waliotoa mchango mkubwa kwa ajili ya wananchi.

Nishani hiyo ni ya heshima ya juu zaidi  kwa wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China. Picha za  nembo ya Chama, nyota yenye pembe tano, bendera, mnara na nuru, alizeti, mlima na mto, na mawingu ya baraka zilizochongwa juu ya nishani zinaashiria majukumu makubwa kwa wanachama.