Idadi ya watu waliokufa kwenye ajali ya kubomoka kwa jengo katika jimbo la Florida imeongezeka hadi 18
2021-07-01 09:07:58| CRI

Miili minne zaidi imepatikana kwenye kifusi cha jengo lililobomoka katika jimbo la Florida nchini Marekani na kufanya idadi ya watu waliokufa katika ajali hiyo kufikia 18.

Meya wa Kaunti ya Miami-Dade Bibi Daniella Levine Cava ametaja idadi hiyo kwenye mkutano na wanahabari, wakati kazi ya utafutaji inaendelea kwa siku saba sasa.

Kufuatia idadi hiyo ya vifo, idadi ya watu wasiojulikana walipo sasa imepungua na kuwa 147, na wale wanaojulikana walipo imekuwa 139.

Licha ya kuwa uwezekano wa kuwaokoa watu wakiwa hai unazidi kuwa mdogo, Kamanda wa zimamoto na uokoaji wa kaunti ya Miami-Dade Bw. Alan Cominsky, amesema wanaendelea na juhudi za utafutaji, lakini ni vigumu kuondoa vipande vikubwa vya kifusi, kwa kuwa vinavunjika kadiri vinavyoondolewa.