China yasema kinachoitwa “uchunguzi wa kutafuta chanzo” unaofanywa na baadhi ya nchi ni udaganyifu wa kisiasa
2021-07-07 09:49:56| cri

 

 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian jana amesema, kile kinachoitwa “uchunguzi wa kutafuta chanzo” cha virusi vya Corona uliofanywa na Marekani na baadhi ya nchi, ni udanganyifu wa kisiasa.

Zhao amesema, ili kukwepa wajibu wao na kuipaka matope China, nchi hizo zinatumia njia zote, ikiwemo kampeni za kuwanyamazisha wanasayansi, na kuongeza kuwa, uchunguzi wa kutafuta chanzo cha virusi hivyo ni suala la kisayansi, ambao unapaswa kufanyika chini ya ushirikiano wa wanasayansi duniani.

Awali, baadhi ya wanasayansi walishikilia uchunguzi wa kutafuta chanzo kwa msimamo wa haki na moyo wa sayansi, lakini wanakabiliwa na shinikizo la kisiasa, dhuluma hata kutishiwa maisha yao.