Rais Xi Jinping apongeza Maadhimisho ya Miaka Mitano tangu kuanzishwa kwa SSCAF na ISSCAD
2021-07-08 14:42:37| Cri

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka Mitano tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Ushirikiano kati ya Kusini na Kusini SSCAF, na Chuo cha Ushirikiano na Maendeleo ya Kusini na Kusini ISSCAD.

Rais Xi ameeleza kuwa, katika miaka mitano iliyopita, SSCAF na ISSCAD zimeonesha umuhimu mkubwa kwa ajili ya kuhimiza ushirikiano kati ya Kusini na Kusini. Pia amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi zinazoendelea duniani na kunufaika kwa pamoja na fursa za kujiendeleza. Anatumai kuwa mashirika hayo mawili yatatoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.