Umoja wa Mataifa wazitaka nchi zilizoendelea kutimiza ahadi yao kwa nchi zinazoendelea kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi
2021-07-09 08:34:18| cri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana ametoa wito kwa nchi zilizoendelea kutimiza ahadi zao za kuzisaidia nchi zinaoendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Bw. Guterres amesema, nchi zilizoendelea zinatakiwa kuweka wazi jinsi zitakavyotoa dola bilioni 100 za kimarekani kila mwaka kwa nchi zinaoendelea, kama ilivyoahidiwa miaka kumi iliyopita.

Pia amesema, misaada kwa nchi zinazoendelea ni lazima, ili kuhimiza maendeleo ya dunia, kurudisha ushirikiano kati ya nchi mbalimbali, na kushinda mapambano dhidi ya janga la COVID-19.