Waraka mweupe kuhusu uhakikishaji wa haki na usawa wa makabila mbalimbali mkoani Xinjiang watolewa
2021-07-14 13:56:28| cri

 

 

Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka mweupe kuhusu uhakikishaji wa haki na usawa wa makabila mbalimbali mkoani Xinjiang.

Waraka huo umesema, mkoa huo unashikilia kanuni za kulinda uhalali wa kuzuia vitendo haramu, kuzuia msimamo mkali, kukinga uingiliaji na kupambana na uhalifu, na kutekeleza kwa pande zote sera ya uhuru wa kidini. Shughuli za kiimani za kawaida zinalindwa kwa kufuata sheria, na haki za uhuru wa kuabudu wa raia zinahakikishwa.

Pia waraka huo umesema, mkoa huo unaendelea kuzidisha uwekezaji katika ujenzi wa maisha ya watu na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na makabila mbalimbali yamepata kwa usawa fursa za kujiendeleza, kujenga kwa pamoja na kufurahia maisha mazuri kwa pamoja, na kwamba haki za kiuchumi nazo zimehakikishwa.