China yalaani Marekani kwa kutoa tahadhari dhidi ya biashara ya Hong Kong
2021-07-18 17:58:10| CRI

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China amelaani Marekani kwa kutoa tahadhari kuhusu mazingira ya biashara katika mkoa wa utawala maalumu wa China Hong Kong, na kuweka vikwazo dhidi ya maofisa ya serikali kuu ya China katika mkoa huo.

Msemaji huyu amesema kitendo hicho cha Marekani kimekiuka sheria ya kimataifa na utaratibu wa kimsingi wa uhusiano wa kimataifa, na kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

Amesisitiza kuwa China siku zote inafuata sera za “Nchi Moja, Mifumo Miwili”, na “Watu wa Hong Kong Kutawala Hong Kong”, tangu kuanza kwa utekelezaji wa sheria ya usalama wa taifa mkoani Hong Kong, utaratibu wa jamii katika mkoa huo umerejeshwa, na mkoa huo umerudi katika njia ya maendeleo, na wageni pia wamepata mazingira mazuri zaidi ya uwekezaji.