Naibu waziri wa mambo ya nje wa China asema Marekani inatakiwa kutatua kwanza suala lake la haki za binadamu
2021-07-26 16:03:06| Cri

Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Xie Feng alipokutana na mwenzake wa Marekani Bi Wendy Sherman ambaye yuko ziarani nchini China, amesema Marekani inatakiwa kutatua kwanza suala lake la haki za binadamu.

Amesema kutoka upande wa historia, Marekani ilifanya mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa kienyeji; kutoka upande wa sasa, hali yake mbaya katika mapambano dhidi ya maambukizi ya COVID-19 yamesababisha vifo vya watu zaidi ya laki 6.2 nchini humo; kutoka upande wa dunia, uchokozi na vita vilivyoanzishwa na Marekani vimeleta maafa kwa dunia nzima.

Mbali na hayo amesema utamaduni wa China unapendekeza kutotishia nchi yoyote. Wakati China ikikabiliwa na uingiliaji kutoka nje, hatua inayochukuliwa na China ni kulipiza kisasi kwa kulingana na halisi na sheria, ili kulinda maslahi halali ya taifa na usawa na haki za kimataifa.