China yasema virusi vya kisiasa navyo vinatakiwa kuchunguzwa chanzo chake
2021-07-26 08:16:08| cri

Waziri wa mambo ya nje ya China Wang Yi, amesema virusi vya Corona vinatakiwa kuchunguzwa chanzo chake na vilevile virusi vya kisiasa pia vinatakiwa kuchunguzwa chanzo chake.

Wang Yi amesema hayo jana alipokutana na wanahabari akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Finland Pekka Haavisto, alipozungumzia maoni ya China kuhusu baadhi ya nchi chache zinazotumia uchunguzi wa virusi vya Corona kama njia ya kuishambulia China. Amesema, uchunguzi wa chanzo cha virusi hivyo ni suala ya kisayansi, na linapaswa kuchunguzwa na wanasayansi ili kuweza kuepusha jamii na hatari za siku za baadaye.

Akizungumzia virusi vya kisiasa vinavyotakiwa kuchunguzwa chanzo chake, Wang Yi amesema Sekretariet ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ilizitaarifu nchi wanachama kuhusu awamu ya pili ya uchunguzi wa chanzo cha virusi vya Corona, ambao umewashangaza wanasayansi kwa kuwa hauendani na mahitaji ya azimio lililopitishwa katika mkutano wa 73 wa Afya wa Dunia, na pia umepuuza matokeo na mapendekezo ya ripoti ya kwanza ya timu ya pamoja ya utafiti.