Wang Yi akanusha kauli zilizotolewa na Marekani na Japan kuhusu China
2021-08-05 08:43:00| Cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekanusha vikali kauli zilizotolewa na Marekani na Japan kuhusu masuala ya Xinjiang na Hong Kong na kuishambulia China kwa kisingizio cha haki za binadamu.

Bw. Wang amesema kauli kama hizo za kupaka matope zimepitwa na wakati na kwamba hazifai kujibiwa hata kidogo na kwamba nchi za ASEAN haziungi mkono, hata hivyo Bw. Wang amesema China ina haki ya kukanusha kwa msingi wa kanuni ya ulipaji.

Wakati masuala yanayohusiana na Xinjiang na Hong Kong ni ya ndani ya China, Bw. Wang amesema kutoa kauli zisizo za uwajibikaji juu ya masuala ya ndani ya China kumekiuka sana kanuni za msingi za utawala za mahusiano ya kimataifa, na kudhoofisha kanuni ya usawa wa kujitawala.