Jopo la washauri bingwa laweka wazi uwezo wa Marekani wa kupambana na janga la COVID-19
2021-08-10 10:34:12| cri

Taasisi ya utafiti wa mambo ya fedha ya Chongyang katika Chuo Kikuu cha Renmin cha China, pamoja na jopo la washauri bingwa la Taihe na Taasisi ya utafiti ya Haiguo Tuzhi, zimetoa ripoti ya utafiti ya “Marekani No 1? Ukweli wa mapambano dhidi ya COVID-19 nchini Marekani” inayoweka wazi kwa dunia ukweli huo unaokanusha madai ya Marekani kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika mapambano hayo .

Ripoti hiyo inahitimisha baada ya kupitia mambo ya halisi kwamba, Marekani ni nchi ya kwanza duniani inayoshindwa kupambana COVID-19, nchi ya kwanza duniani inayolaumu nchi nyingine kisiasa, inayoongoza kwa maambukizi, inayokabiliwa na mgawanyiko wa kisiasa, inayoongoza duniani kwa kutoa fedha nyingi kukabiliana na athari za COVID-19, nchi ya kwanza duniani yenye msukosuko katika kipindi cha maambukizi, isiyotoa taarifa za kweli, na nchi ya kwanza duniani yenye mizizi ya ugaidi.

Martin Jacques, mtafiti mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza, amesema serikali na vyombo vya habari vya nchi za magharibi havijaweka wazi mafanikio ya China ya kushinda janga hilo, ili kujaribu kugeuza ufuatiliaji wa umma kutokana na nchi hizo kushindwa kukabiliana vizuri na janga hilo.

William Jones, mkuu wa ofisi ya Washington ya jarida la Marekani la Executive Intelligence Review, amesema virusi vya Corona vimegeuzwa kuwa silaha ya kisiasa iliyotumiwa na serikali iliyopita ya Marekani chini ya rais Donald Trump kushambulia na kuzuia maendeleo ya China na kuzuia China kutoa mchango katika maendeleo ya dunia.

Tu Wenxiao, naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Ufuatiliaji, Tahadhari ya Mapema na Tathmini ya Hatari ya Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa ya China, amesema wanasayansi wenye ujuzi duniani kote, wataalamu wa kisiasa wa Marekani na hata baadhi ya wakurugenzi wa zamani wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa ya Marekani, mwaka jana, waliishutumu nchi hiyo kwa kushindwa kupambana na janga hilo. Amesema, kutolewa kwa ripoti hiyo ni hatua muhimu sana, ambayo imetathmini kikamilifu suala la kinga na udhibiti wa janga la COVID-19 nchini Marekani.