Kesi ya rushwa ya Zuma yaahirishwa hadi Septemba
2021-08-11 09:43:14| cri

Jaji Piet Koen wa Mahakama ya Juu ya Pietemaritzburg iliyoko KwaZulu-Natal amesema, kesi ya rushwa na utakatishaji wa pesa inayomkabili rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma imeahirishwa hadi Septemba 9 na 10 mwaka huu baada ya Bw. Zuma kulazwa hospitali.

Hatua hiyo imekuja wakati Zuma akitumikia kifungo cha miezi 15 jela kwa kosa la kudharau mahakama.

Jaji Koen aliamuru timu ya wanasheria ya Zuma kuwasilisha ripoti ya matibabu ya Bw. Zuma kabla ya Agosti 20 ili kutoa ufafanuzi juu ya afya yake na kama ataweza kufikishwa mahakamani. Pia aliamuru kwamba serikali inaweza kuteua daktari wake kumfanyia uchunguzi Bw. Zuma.