Mwanaharakati wa Afrika atoa wito wa kuwalinda Simba wanaokumbwa na tishio kubwa
2021-08-11 10:49:41| CRI

Jana ilikuwa ni Siku ya Simba Duniani, meneja wa kampeni za wanyamapori katika ofisi ya Afrika ya Shirika la uhifadhi wa wanyama duniani Bibi Edith Kabesiime, amesema Simba wa Afrika wanakumbwa na matishio mbalimbali, na wanahitaji kulindwa zaidi.

Kabesiime amesema Simba wanakabiliwa na changamoto zinazotokana na binadamu na tabianchi, ambapo uhai wa Simba hao unatishiwa na vitendo kadhaa ikiwemo ujangili, kupoteza makazi yao, uhaba wa chakula, na kushambuliwa na wafugaji kwa kulipiza kisasi.

Takwimu kutoka Shirika la Uhifadhi wa Wanyama Duniani zimeonyesha kuwa, kwa sasa idadi ya Simba barani Afrika ni takriban elfu 20, idadi ambayo imepungua ikilinganishwa na idadi ya milioni 2 ya miaka 100 iliyopita. Pande husika zinapaswa kuchukua hatua ili kukabiliana na changamoto hiyo.