Wanajeshi 25 na raia 7 wa Algeria wafariki kutokana na moto wa msituni
2021-08-11 09:41:15| cri

Wizara ya Ulinzi ya Algeria imesema wanajeshi wasiopungua 25 wamepoteza maisha yao wiki hii wakati walipojaribu kuzima moto wa msituni unaoenea katika majimbo ya Tizi Ouzou na Bejaia, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Inasema moto huo ulianzia usiku wa Jumatatu wiki hii katika majimbo 14 ya Algeria kwa wakati mmoja na kusababisha raia wasiopungua saba kufa na wengine wengi kujeruhiwa. Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo inasema inawezekana tukio hilo limesbabishwa na“kitendo cha jinai".

Mapema Jumanne waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Kamel Beldjoud alitaka mamlaka husika kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha moto huo na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria, huku akihakikisha kuwa serikali itawafidia wakazi walioathiriwa na moto huo, ambapo ujumbe wa wataalamu 140 utatumwa kwenye jimbo la Tizi Ouzou kutathmini kiwango cha hasara iliyosababishwa na moto huo.