Afrika Kusini kuweka vizuizi vya uvuvi ili kuzuia kutoweka kwa penguins wa kiafrika
2021-08-12 09:44:22| cri

Afrika Kusini itaweka vikwazo kwa uvuvi karibu na makazi 6 ya penguins baada ya idadi yao kupungua.

Habari zinasema, mashirika mengi ya kuhifadhi wanyama nchini Afrika Kusini yameona kwamba, penguins wa kiafrika huenda watatoweka nchini humo ndani ya miaka 14 kama hatua kali hazitachukuliwa.