Serikali ya Nigeria kuondoa marufuku dhidi ya Twitter
2021-08-12 09:38:23| cri

 

 

Wizara ya Habari na Utamaduni ya Nigeria jana imesema, mazungumzo kati ya serikali ya nchi hiyo na kampuni ya Twitter yanakaribia kukamilika, na marufuku dhidi ya Twitter itaondolewa.

Wizara hiyo imesema, pande hizo mbili zimefikia maoni ya pamoja kwenye baadhi ya maeneo, na makubaliano yanatarajiwa kufikiwa ndani ya siku au wiki chache zijazo.

Juni 2 mwaka huu, Twitter ilifuta ujumbe wa Rais Mohammadu Buhari wa Nigeria kuhusu onyo la "Harakati ya Biafra", na tarehe 5 mwezi huo huo, serikali ya Nigeria ilisitisha matumizi ya mtandao wa Twitter nchini humo.