Hasara iliyosababishwa na mlipuko wa kituo cha uzalishaji umeme cha Medupi nchini Afrika Kusini yakadiriwa kufikia rand bilioni 20
2021-08-12 09:58:27| cri

 

Wataalamu wa nishati wa Afrika Kusini wamesema, hasara iliyosababishwa na mlipuko uliotokea tarehe 8 mwezi huu katika Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Medupi nchini humo inakadiriwa kufikia rand za Afrika Kusini kati ya bilioni 20 hadi 40, na huenda ikachukua zaidi ya mwaka mmoja kuboresha mashine iliyoharibika.

Msemaji wa kampuni ya umeme ya Afrika Kusini (ESKOM) Sikonathi Mantshantsha amesema, kampuni na wachunguzi husika wanafanya uchunguzi na tathmini, na kwa sasa bado hawawezi kuthibitisha uharibifu wa mashine na muda unaohitajika kwa matengenezo.