Kenya yapanga kuchochea uwekezaji kwenye makampuni yanayojishughulisha na bidhaa za maji
2021-08-12 09:15:19| CRI

Kenya itahamasisha mitaji, teknolojia na nguvu kazi kutoka sekta mbalimbali na kwa wakopeshaji, ili kuchochea ongezeko kwa makampuni yanayojihusisha na shughuli za maji na kupanua upatikanaji wa bidhaa zake.

Ofisa mkuu mtendaji wa Mfuko wa maendeleo ya sekta ya Maji Bw. Ismail Fahmy Shaiye, amesema serikali ya Kenya itatoa kipaumbele kwa uwezo endelevu wa makampuni yanayotoa huduma ya maji, ili kuharakisha upatikanaji kwa wote wa maji safi ya kunywa, na kiwango cha msingi cha usafi.

Amesema kuna sera na sheria zinazohimiza sekta binafsi kufadhili mashirika ya maji, ili kuhakikisha yanakuwa na uwezo wa kutosha kufikia malengo ya kufikisha maji kwa watu wote. Pia amesema Kenya imevutia uwekezaji na mikopo kwenye sekta ya maji, kufuatia mageuzi yaliyobadilisha uwekezaji kwenye sekta hiyo.