Vijana wa Kenya wahimiza kuwepo kwa mfumo wa jamii kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira
2021-08-12 09:15:44| CRI

Makundi kadhaa yanayowakilisha vijana nchini Kenya yameitaka serikali kuweka mfumo wa jamii unaoweza kuisaidia jamii kutokana na tatizo la kukosekana kwa ajira, linalotokana na mabadiliko ya idadi ya watu.

Kwenye kongamano moja lililofanyika mjini Mombasa, makundi hayo yameitaka serikali kuharakisha mageuzi yatakayohimiza kuwawezesha vijana hasa katika kipindi hiki ambacho kuna changamoto za janga la Corona.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2020 kutoka shirika la leba la Umoja wa Mataifa (ILO) kiasi cha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana wa Kenya wenye umri wa kati ya miaka 18 na 35 ambao ni asilimia 35 ya wakenya wote, kilikuwa asilimia 7.2.

Mwenyekiti wa harakati ya United Green Movement Bw. Moses Gichuho, amesema sera nzuri, pamoja na mafunzo ya ufundi kazi yanazingatia soko, ni muhimu katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.