Zanzibar yaripoti vifo vya watu 15 kutokana na COVID-19
2021-08-12 08:52:53| CRI

Zanzibar imeripoti vifo vya watu 15 walioambukizwa ugonjwa wa COVID-19 katika miezi miwili iliyopita.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Zanzibar Bw. Nassor Ahmed Mazrui amesema watu 390 waliripotiwa kuambukizwa COVID-19 katika hospitali za Zanzibar katika kipindi hicho.

Bw. Nassor amewaambia waandishi wa habari kwamba miongoni mwa wagonjwa hao 390 wa COVID-19, ambao ni pamoja na wenyeji 112 na wageni 278, watu 207 wamepona.

Amewakumbusha wananchi kufuata kwa makini miongozo iliyotolewa kwa umma kujikinga dhidi ya janga la COVID-19 ili kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huo, na wanapaswa kuepuka kushikana mikono na  mikusanyiko ya watu wengi, na kuvaa barakoa.