Jumuiya ya wawekezaji ya Kenya yahimiza uwepo wa uvumbuzi unaoongozwa na vijana ili kuharakisha hali ya kufufuka kwa uchumi
2021-08-13 09:02:14| CRI

Ofisa wa jumuiya ya kuhimiza ajira kwenye sekta binafsi ya Kenya Bw. Ehud Gachugu amesema ili kufikia malengo ya ufufuaji wa uchumi ulio shirikishi, kuna haja ya kuwepo kwa uwekezaji wa kutoka kwa uvumbuzi unaoongozwa na vijana.

Bw. Gachugu amesema kuwekeza kwenye teknolojia kwa makampuni yanayomilikiwa na vijana kutahimiza ongezeko la uchumi, usalama wa chakula, kudhibiti magonjwa na kuzoea mabadiliko ya tabia nchi.

Amependekeza kuwepo kwa misaada ya moja kwa moja na mikopo yenye riba nafuu kwa makampuni yanayomilikiwa na vijana, ambayo yanalenga kutatua changamoto za kiuchumi, kijamii na kimazingira zinazotokana na janga la COVID-19.

Lakini pia amependekeza vijana wavumbuzi kuwekwa karibu na watu waliopata mafanikio mbali na kuhimiza uwezo wao kuleta mabadiliko kwenye sekta muhimu za uchumi kama kilimo, nishati na huduma za fedha.