China yasema iko tayari kuchangia kwenye amani ya kudumu nchini Somalia
2021-08-13 09:01:47| CRI

China imesema iko tayari kutoa mchango chanya kwenye kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana nchini Somalia.

Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing, amesema China iko tayari kufanya kazi pamoja na jumuiya ya kimataifa kutoa mchanga chanya ili amani ya kudumu na maendeleo endelevu vipatikane nchini Somalia.

Akiongea kwenye mkutano wa baraza la usalama kuhusu hali katika pembe ya Afrika, balozi Dai amesema hali ya kisiasa nchini Somalia imekuwa kwenye mwelekeo mzuri, na China inakaribisha makubaliano yaliyofikiwa na pande mbalimbali za Somalia kwenye kuendelea na mchakato wa uchaguzi, na kufanya uchaguzi kama ilivyokubaliwa kwenye ratiba ya uchaguzi.

Hata hivyo amesema hali ya nchi hiyo bado ina changamoto, hasa kutokana na kundi la Al Shabaab kuendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya raia wasio na hatia, ujumbe wa umoja wa Afrika AMISOM na majeshi ya Somalia.