Upigaji kura kwenye uchaguzi mkuu wa Zambia waanza
2021-08-13 11:02:30| CRI

Upigaji kura kwenye uchaguzi mkuu wa Zambia ulianza rasmi jana asubuhi, na vituo zaidi ya elfu 12 vya kupigia kura kote nchini vilifunguliwa kwa wakati mmoja kwa wapiga kura milioni 7 waliojiandikisha.

Uchaguzi huo unashirikisha uchaguzi wa rais, wabunge, serikali za mikoa na mitaa pamoja na mameya. Matokeo ya uchaguzi huo yatatolewa ndani ya saa 72 baada ya kumalizika kwa upigaji kura.

Uchaguzi mkuu wa Zambia unafanyika kila baada ya miaka mitano. Katiba ya nchi hiyo inasema mshindi wa uchaguzi anatakiwa kupata zaidi ya nusu ya kura zote, na kama hakuna mshindi kwenye duru ya kwanza, wagombea wawili wanaoongoza wataingia kwenye duru ya pili ya upigaji kura.