Sudan, ICC zasaini makubaliano ya kutimiza haki kwenye eneo la Darfur
2021-08-13 09:03:34| CRI

Serikali ya Sudan na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC wamesaini hati ya maelewano (MoU) kuhusu utoaji wa taarifa na utimizaji wa haki kwa wahanga wa machafuko kwenye eneo la Darfur, Sudan.

Waziri wa Sheria wa Sudan Bw. Nasredeen Abdelbari alisaini makubaliano hayo na mwendesha mashtaka wa ICC Bw. Karim Khan.

Akikutana na wanahabari mjini Khartoum, Bw. Khan amesema ujumbe wa ICC na serikali ya Sudan walishindwa kufikia mwafaka kuhusu tarehe halisi ya kuwakabidhi kwa ICC rais Omar al-Bashir aliyeondolewa madarakani na washukiwa wengine, akiongeza kuwa ICC itafungua ofisi ya kudumu mjini Khartoum.

Ofisa huyo pia hakuondoa uwezekano wa kesi ya al-Bashir na washukiwa wengine kusikilizwa nchini Sudan chini ya usimamizi wa ICC.