Africa CDC: Nchi za Afrika zimepata dozi milioni 114 za chanjo ya COVID-19
2021-08-13 11:03:03| CRI

Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika Africa CDC kimesema, hadi sasa, nchi 53 za Afrika zimepata dozi milioni 114 za chanjo ya COVID-19.

Kituo hicho kimesema asilimia 1.75 hivi ya watu wote barani Afrika wamekamilisha kupewa dozi kamili za chanjo hiyo.

Pia kimesema hadi sasa dozi milioni 77.3 kati ya dozi zote milioni 114 zimeshatolewa kwa watu.

Kituo hicho kimeongezeka kuwa nchi tano Morocco, Afrika Kusini, Misri, Nigeria na Tunisia zimetoa dozi nyingi zaidi za chanjo kwa wananchi wao.