Watu 10 wauawa katika mapigano kati ya jeshi linalounga mkono serikali ya Yemen na wapiganaji wa kundi la Houthi
2021-08-16 08:33:21| CRI

Watu 10 wameuawa katika mapigano kati ya jeshi linaloiunga mkono serikali ya Yemen na waasi wa kundi la Houthi yaliyotokea jana katika mji wa pwani wa Hodidah.

Chanzo cha habari ambacho hakikutaka kutaja jina kimeliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, mapigano hayo yametokea katika wilaya ya Tuhyata mjini Hodeidah na kusababisha vifo vya wapiganaji saba wa kundi la Houthi na askari watatu wa jeshi la Yemen.

Mji wa Hodeidah umeshuhudia hali tete ya makubaliano ya kusimamisha mapigano kati ya jeshi la Yemen na kundi la Houthi tangu pande hizo zilipofikia makubaliano ya kusimamisha mapigano chini ya uratibu wa Umoja wa Mataifa mjini Stockholm, Sweden, mwezi Desemba, 2018.