Kiongozi wa upinzani wa Zambia ashinda uchaguzi wa Rais wa Zambia
2021-08-16 14:46:25| Cri

Kiongozi wa upinzani wa Zambia Bw. Hakainde Hichilema amekuwa mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa uliofanyika Agosti 12, baada ya kumshinda Rais aliye madarakani Bw. Edgar Lungu.

Bw. Hichilema amefanikiwa kupata zaidi ya asilimia 51 ya kura, kwa kupata kura 2,810,757 huku Bw. Lungu akipata kura 1,814,201.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zambia Jaji Esau Chulu ametangaza matokeo hayo baada ya kupitia kwa makini matokeo kutoka majimbo 155 kati ya majimbo 156.

Kulikuwa na jumla ya wagombea 16, kwenye uchaguzi uliovutia asilimia 70 ya wapiga kura kati ya zaidi ya milioni 7 waliojiandikisha. Bw. Hichilema ni mfanyabiashara tajiri ambaye alishindwa kwenye chaguzi 5 zilizopita. Sasa amekuwa rais na kazi yake kubwa itakuwa kufufua uchumi, ajenda ambayo aliitilia mkazo wakati wa uchaguzi.