Wakenya milioni 2.1 wakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula
2021-08-18 08:47:05| CRI

 

 

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema hivi sasa Wakenya milioni 2.1 wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula kutokana na maafa ya ukame, idadi hiyo ilikuwa milioni 1.4 mwezi Februari.

Katibu mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya Bibi Asha Mohammed,amesema watu walioathirika wako katika wilaya 12 zenye ukame, na hali mbaya ya chakula na lishe inatokana na uhaba wa mvua katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka jana na miezi ya Machi, Aprili na Mei ya mwaka huu. Ameongeza kuwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa, hali ya ukosefu wa usalama wa chakula itaathiri wilaya 20.

Bibi Mohammed anaona upungufu wa maji na ufugaji unachochea migogoro kati ya wahamiaji, na kuzidisha hali ya utapiamlo katika sehemu ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.