China kuendelea kushirikiana na pande mbalimbali husika kuhimiza Afghanistan kusimamisha vita haraka iwezekanavyo
2021-08-18 08:39:17| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying, amesema China inaendelea kuwasiliana na pande mbalimbali husika, kuhimiza Afghanistan kusimamisha vita haraka iwezekanavyo, na kutimiza amani ya kudumu.

Bibi Hua Chunying amefafanua kazi ya China katika kuhimiza usuluhishi wa amani wa Afghanistan, na kusema msimamo wa China ni kuheshimu uhuru wa mamlaka na ukamilifu wa ardhi wa Afghanistan, kushikilia kutoingilia mambo ya ndani ya Afghanistan na kutekeleza sera ya kirafiki kwa watu wote wa Afghanistan.

Pia amesema China inalihamasisha kundi la Taliban kufuata sera ya kidini iliyo madhubuti, kushirikiana na pande mbalimbali kuunda muundo wa kisiasa ulio wazi na wenye msikilizano, kutekeleza sera ya amani na kirafiki ya mambo ya nje, hasa kuishi kwa masikilizano na nchi jirani, na kutimiza ukarabati na maendeleo ya nchi hiyo. Pia amekumbusha kuwa mamlaka mpya ya Afghanistan inapaswa kujitenga na makundi ya kigaidi, kuzuia na kupambana na makundi la kigaidi likiwemo Kundi la harakati ya kiislam la Turkustan Mashariki, ili kuzuia Afghanistan isiwe sehemu yenye makundi yenye msimamo mkali ya kigaidi.