Mwenyekiti mpya wa SADC alalamikia kukosekana kwa usawa katika upatikanaji wa chanjo ya COVID-19
2021-08-18 08:40:43| CRI

Rais Lazarus Chakwera wa Malawi ambaye ni mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), amelalamikia kutokuwepo kwa usawa kwenye upatikanaji wa chanjo ya COVID-19 duniani.

Akiongea jana mjini Lilongwe baada ya kuchukua uenyekiti wa SADC kwenye mkutano wa kawaida wa jumuiya hiyo, Bw. Chakwera alisema kukosekana kwa usawa ni lazima kushughulikiwe, kwani kunakwamisha juhudi za kuokoa maisha ya mamilioni watu katika eneo la SADC.

Amesema nchi za Afrika ni wanachama kamili wa jumuiya ya dunia, na kwamba waafrika wana wajibu wa kukataa kuchukuliwa kama watu wa daraja la pili, kwa ajili ya utu wa binadamu duniani kote.