Watu 47 wakiwemo raia 30 wauawa kwenye shambulizi nchini Burkina Faso
2021-08-19 08:04:50| CRI

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mawasiliano ya Burkina Faso inasema watu 47 wakiwemo raia 30, wanajeshi 14 na askari watatu wa akiba, wameuawa kwenye shambulizi lililotolea jana nchini humo.

Taarifa inasema msafara wa pamoja wa raia, kikosi cha ulinzi na usalama na watu wanaojitolea kulinda taifa VDP walishambuliwa katika eneo la Gorgadji la nchi hiyo. Taarifa inaongeza kuwa, kazi ya uokoaji inaendelea.

Habari zinasema hali ya usalama nchini Burkina Faso imekuwa mbaya zaidi tangu mwaka 2015, ambapo magaidi wamewaua watu zaidi 100 na kusababisha watu milioni 1 kupoteza makazi yao.