China ni miongoni mwa maeneo 10 ya Ethiopia kuuza kahawa katika mwezi Julai
2021-08-19 11:18:24| Cri

Mamlaka ya Usimamizi wa Kahawa na Chai ya Ethiopia jana ilisema kuwa mapato na uuzaji wa kahawa, chai na viungo katika nchi za nje vimefikia kiwango cha juu kuliko lengo la mwezi Julai lililopangwa.

Mamlaka hiyo ilisema kuwa Ethiopia ilipanga kuuza tani 22,487.08 za kahawa, chai na viungo mwezi Julai na kupata dola za kimarekani milioni 73.38, lakini ilipata zaidi ya dola za kimarekani milioni 116.63 kwa kusafirisha tani 31,939.10 za bidhaa, na uuzaji katika nchi za nje na mapato yaliongezeka. China ilikuwa mojawapo ya nchi 10 zilizonunua zaidi.