Gazeti la Herald: Afrika yapaswa kukataa mchezo wa kuufanya utafutaji wa chanzo cha virusi vya Corona kuwa wa kisiasa
2021-08-19 11:17:36| Cri

Makala iliyochapishwa jana na gazeti la Herald la Zimbabwe inasema, Afrika ambayo inakabiliwa na kiwango cha chini cha utoaji wa chanjo ya COVID-19, inatakiwa kuifuata China ambayo ni mfano wa suluhisho lenye ufanisi kwa janga la Corona.

Makala hiyo imeihimiza Afrika kukataa mchezo wa kulifanya suala la kutafuta chanzo cha virusi vya Corona kuwa la kisiasa, ikisisitiza kuwa kama vita hivi vya upotoshaji vikiruhusiwa kuendelea, bara la Afrika litaendelea kukabiliwa na mateso. Pia imesema hakuna sababu ya maana ya kufikiria sana chanzo chake, haswa kama ukweli wake ni mchezo wa siasa.

Makala hiyo pia imebainisha kuwa kinachohitajika kwa Afrika kupambana na janga hilo ni majawabu yanayotekelezeka, na wala sio vita vya propaganda. Imeongeza kuwa Afrika inapaswa kuepuka kutumiwa na Marekani kuishutumu China kuwa chimbuko la virusi vya Corona, na badala yake bara hilo linapaswa kuzingatia kuimarisha mshikamano wa dunia ili kupata suluhisho la kudumu kwa janga la Corona.