Watu 43 wafariki kutokana na mvua kubwa na mafuriko nchini Sudan
2021-08-20 08:55:46| cri

Serikali ya Sudan imesema nchi hiyo imekumbwa na mvua kubwa na mafuriko hivi karibuni, ambayo yamesababisha vifo vya watu 43 na maelfu ya nyumba kuporomoka.

Tume ya taifa ya ulinzi wa raia ya Sudan, imesema jimbo la Kaskazini ndilo lililoathiriwa vibaya zaidi, huku watu 23 wamefariki. Aidha, nyumba 2,800 zimeporomoka kabisa, na zaidi ya nyumba 8,600 zimeathiriwa kiasi.

Tume hiyo pia ilisema, sehemu ya kusini mwa nchi hiyo inatarajiwa kuwa na mvua itakayoendelea kunyesha katika siku za usoni, na watu wa eneo hilo bado wanahitaji kuwa waangalifu.