China yaadhimisha miaka 70 ya ukombozi wa amani wa Tibet
2021-08-20 10:48:57| Cri

China imefanya maadhimisho ya kusherehekea miaka 70 ya ukombozi wa amani wa Tibet. Hafla hiyo ilifanyika huko Lhasa, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Tibet.

Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC Bw. Wang Yang alihudhuria mkutano huo na kuwasilisha salamu za pongezi. Amesema kuwa ukombozi wa amani wa Tibet uliopatikana mwaka 1951 ni ushindi mkubwa katika ukombozi wa watu wa China na kuunganika tena kwa China, akiongeza kwamba ilionyesha mabadiliko ya kihistoria na umuhimu wa Tibet, na kwamba pamoja na nchi nzima, Tibet, kama ilivyotarajiwa, imekamilisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote.