Misri kutoa chanjo ya COVID-19 ya CoronaVac ya China inayotengenezwa nchini humo
2021-08-23 08:47:19| Cri

Misri kutoa chanjo ya COVID-19 ya CoronaVac ya China inayotengenezwa nchini humo_fororder_3

Waziri wa afya na watu wa Misri Bibi Hala Zayed ametangaza kuwa Misri itaanza kuvipatia vituo vyake chanjo ya COVID-19 ya CoronaVac ya China inayotengenezwa nchini humo ndani ya siku mbili. Kwa mwezi chanjo hizo zitatengenezwa na kufikia milioni 15 hadi 18.5.

Zayed amesema inakadiriwa kuwa idadi ya wagonjwa wanaothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Misri itaongezeka tena kuanzia katikati ya nusu ya pili ya mwezi Septemba. Wizara ya afya itawapatia wananchi chanjo haraka iwezekanavyo. Amesisitiza kuwa watumishi wa afya na wafanyakazi wa serikali nchini humo wanapaswa kupata chanjo kabla ya mwezi Oktoba.